Habari
Rais Samia Atembelea kituo cha kupooza umeme Katavi
Rais Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan ametembelea kituo cha kupokea ,kupoza na kusambaza umeme ya gridi ya taifa cha Iyonga Mkoani Katavi
Pia Dkt Samia amepokea taarifa kuhusu kituo hicho cha kupokea , kupoza na kusambaza umeme wa gridi ya taifa kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi Gissima Nyamo Hanga.
Rais Dkt. Samia anaendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani humo ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi.