Habari

Rais Samia atoa maagizo suala la machinga (Video)

RAIS Samia Suluhu Hassan ameelekeza Wakuu wa Mikoa kuchukua hatua zinazostahili katika zoezi la kuwapanga wamachinga nchi nzima bila kuleta vurugu, fujo na uonevu.

Rais Samia amesema tendo la wamachinga kuonekana kila pahala hasa mbele ya milango ya maduka kunasababisha serikali kushindwa kukusanya mapato kwa kuwa wenye maduka ambao ndio walipa kodi hushindwa kufanya biashara.

“Najua kwamba serikali tumetoa fursa kubwa kwa ndugu zetu kufanya shughuri. Watu hawa wamekuwa wakifanya kazi katika maeneo tofauti tofauti.

Wakuu wa Mikoa wanawapanga Wakuu wa Wilaya wanawapanga. Lakini pia kumekuwa na laxity (watu wamepumzika) wameenea kila pahali mpaka kwenye maduka wao wanaziba maduka hayauzi wao wanauza. Baadhi ya wenye maduka wanatoa bidhaa ndani na kuwapatia machinga kuuza kwa sababu watu hawaingii ndani.

-Tendo hili linatukosesha kodi kwa sababu mwenye duka analipa kodi na machinga halipi. Wito wangu kwa Wakuu wa Mikoa mkawapange vyema. Sitaki kuona yale ninayoyaona kwenye tv.R

Related Articles

Back to top button