Habari

Rais Samia awasili Songwe kuendelea na kampeni za uchaguzi mkuu

Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa  Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe kwa ajili ya muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho mkoani Songwe.

Kampeni hizo zinatarajiwa kuendelea mkoani Songwe leo Septemba 03, 2025 ambapo Rais Samia anatarajiwa kuzungumza na wakazi wa mkoa kwa kunadi sera za chama chake.

Mgombea wa Nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Songwe kwa ajili ya muendelezo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama hicho mkoani Songwe tarehe 03 Septemba, 2025.

 

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents