Rais Samia kufanya ziara ya kikazi nchini China
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini China kuanzia leo Septemba 2 hadi Septemba 6, 2024 kushiriki mkutano wa wakuu wa nchi na SErikali wa JUkwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika jijini Beijing.
Kwa mujibu wa taarifga iliyotolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharika Nyanga imesema wakati wa ziara hiyo Rais Samia atakutana na mwenyeji wake Rais wa China Xi Jinping kwa mazungumzo yanayolenga kuimarisha uhusiabno mzuri na wa kihistoria kati ya Tanzania na China ulioasisiwa miaka 60 iliyopita.
Taarifa hiyo imeeleza marais hao wawili pamoja na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema watashiriki na kushuhudia uwekaji saini wa hati za makubaliano ya boreshaji wa Reli ya TAZARA.
Pamoja na mambo mengine miongoni mwa maeneo yanayotarajiwa kupewa kipaumbele kwenye mkutano wa FOCAC ni uendelezaji wa miundombinu, kukuza uwekezaji, uendelezaji wa viwanda, kilimo cha kisasa, amani na usalama, Rais anatarajia kuwa miongoni mwa wakuu wa nchi watakaohutubia ufunguzi wa mkutano wa FOCAC akizungumza kwa niaba ya Kanda ya Afrika Mashariki,” ameeleza Nyanga katika taarifa hiyo.
Aidha taarifa hiyo imeeleza pembezoni mwa mkutano huo, katika kukuza biashara na uwekezaji, Rais Samia atakutana na kampuni na wawekezaji kutoka China kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji zaidi nchini Tanzania.
Written by Janeth Jovin