Habari

Rais Samia kuzindua daraja la JP Magufuli- Kigongo Busisi Mei, mwaka huu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua Daraja la Kigongo Busisi jijini Mwanza mwezi Mei mwaka huu, tayari kwa matumizi ikiwa ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kielelezo na ya kimkakati iliyokamilishwa na Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha, daraja hilo lenye urefu wa kilometa tatu ni kati ya madaraja makubwa Afrika mashariki na kati na linaunganisha Mkoa wa Mwanza na Geita ambapo linachochea ukuaji wa
uchumi kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega, Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka fedha 2025/26.

Ulega ameliambia Bunge kuwa Serikali pia inatekeleza ujenzi wa Daraja la Pangani na barabara za mzunguko zinazojengwa mkoani Dodoma.

Amempongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa usimamizi wake mzuri wa shughuli za Serikali. Kadhalika ameeleza kuwa ndani ya miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan,Serikali pia imekamilisha ujenzi wa mtandao wa barabara za lami wa urefu wa kilometers 1365 Suala ambalo limeendeleza dhamira ya kuhakikisha kuwa barabara zote nchini zinapatikana kwa nyakati zote

Ameeleza kuwa kupitia maoni na michango ya wabunge takriban 20 waliochangia hotuba ya Bajeti ya Waziri Mkuu upande wa miundombinu amepokea maombi mengine mapya ya ujenzi wa barabara Suala ambalo tayari Serikali imeshanza kuyafanyia kazi maombi hayo ya Wabunge.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents