Habari

Rais Samia Suluhu aupiga tafu mradi wa maji wa Kemondo – Maruku kwa kutoa mil 420, Waziri Aweso athibitisha (+ Video)

Waziri wa Maji amefika na kujionea hali ya Mradi wa maji Kemondo-Maruku Wilayani Bukoba, Katika ziara hiyo Mh. Waziri ametembelea ujenzi wa Tanki la lita milioni tatu(3000m3) ambao kwa sasa utelezaji wake upo 35% .


Mradi huo unatarajia kuhudumia wananchi wapatao 117,561 katika kata 6 zenye jumla ya vijiji 17.

Aidha Aweso papo kwa hapo amepiga simu na kumuagiza Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Mfuko wa taifa wa Maji kuhakikisha analeta kiasi cha Tsh.420,000,000 anazodai mkandarasi ili akamilishe ujenzi wa Tanki hilo kwa wakati.

Katika hatua nyingine viongozi wa Wilaya ya Bukoba na mkoa wa Kagera wameipongeza Serikali chini ya Rais Mh.Samia Suluhu Hassan kwa hatua ya kuwaletea mradi wa kimkakati wenye thamani ya Tsh.Bil.15.8 ambao utasaidia kupunguza hadha ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa vijiji hivyo.

Related Articles

Back to top button