Rais Samia Suluhu: Tusiwape mdomo wa kusema tunaminya Uhuru wa Vyombo vya habari, kanuni zifuatwe (+ Video)

“Nasikia kuna vyombo vya habari vilivyofungiwa fungiwa na TV za mikonononi, vifungulieni na vifuate sheria na muongozo wa serikali”.

“Tusiwape mdomo wa kusema kuwa tunaminya uhuru wa vyombo habari.” Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ni muhimu kusimamia vyombo vya habari vya ndani.

“Tusifungie tu kibabe, wafungulieni lakini hakikisha wanafuata miongozo ya serikali”.
Rais Samia ametaka hakikisho kuwa kila atakayepewa ruhusa ya kuendesha chombo cha habari anafuata sheria za serikali na kanuni ziwe wazi kuwa kosa ili adhabu yake ilingane na adhabu inayotolewa.

Rais Suluhu aliyasema hayo katika hafla ya kuwaapisha makatibu wakuu na manaibu wao na viongozi wa taasisi katika ikulu ya Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button