Rais Trump awashambulia Facebook, Twitter na Google ‘mnapunguza followers wangu, nataka maelezo’
Rais wa Marekani, Donald Trump ameituhumu mitandao ya kijamii ya Twitter, Facebook na Google kuwa inamfanyia mchezo mchafu wa kupunguzawafuasi wake (Followers) kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.
Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter, amesema mtandao huo kwa sasa unafanya figisu figisu za kuzuia followers wasiongezeke kwenye ukurasa wake.
“Facebook, Twitter na Google mmekuwa na upendeleo sana tena kwa watu wa (Democratic) hii ni mbaya. Twitter nao wamefanya akaunti yangu watu washindwe kunifikia kwa urahisi. Kuna baadhi ya majina (Followers) yanapunguzwa tuu, lakini mnasema hamjafanya chochote,“ameandika Trump.
Mzee Trump ni moja ya marais maarufu zaidi duniani wanaotumia mitandao ya kijamii kutoa taarifa zao, na hata muda mwingine kuwashambulia wapinzani wake wa kisiasa.