Rais TUCTA aonya siasa kutumika sekta ya afya

Rais wa Shirikisho huru la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Ndg. Tumain Nyamhokya amewataka wanasiasa kuacha kujibu hoja za wafanyakazi wa sekta ya Afya kwa kutumia majukwaa.

Akifunga Semina ya Waajiri na viongozi wa matawi iliyoandaliwa na Chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na Afya TUGHE, ndg. Tumain Nyamhokya amesema kuwa kada ya Afya haipaswi kufanyiwa siasa na hata maamuzi yake yanapaswa kutazamwa kwa jicho la tatu ili kuweza kutenda haki kwa wauguzi na Madaktari.

Amesisitiza kuwa TUGHE inapaswa kulinda wafanyakazi wake na sio kuwaachia maamuzi yao yafanywe na wanasiasa kama vile ambavyo Waziri mwenye dhamana ya Utumishi wa Umma, Mohammed Mchengerwa anavyopambana kuhakikisha haki za watumishi na wafanyakazi zinapatikana.

“Msiruhusu kuonewa. Hatuwalindi wafanyakazi wakorofi na wasio na nidhamu. Lakini hakikisheni wafanyakazi wanaheshimiwa. Waziri Mchengerwa na Naibu wake mambo wanayoyasema tulipaswa tuseme sisi. Wanakemea na kuchukua hatua wanapokuta watumishi wananyanyaswa”. Nyamhokya.

Mwenyekiti TUGHE mkoa wa Arusha, Titho Cholobi.

Ameongeza “Viongozi naomba tushuke chini kupeleka huduma watu wajiandikishe
Simamieni Makatibu waingize wanachama, kingine muwe wamoja ondoeni maneno maneno”.

Kwa upande wa Makatibu wa mabaraza ya vyama amewataka kuhakikisha bajeti zinazopitishwa na bunge zinasimamia stahiki za wafanyakazi na huku akitolea mfano wa sare za wafanyakazi kama vile manesi na madaktari.

Kwa upande wa Katibu Mkuu kutoka TUGHE Ndg. Henry Mkunda amesema katika semina hiyo ya sikubtano, wajumbe wa Semina hiyo wamefundishwa, Maadili ya utumishi wa umma kazini, Utaratibu wa kukuta rufaa pale ambapo watakuwa wamepatiwa maamuzi ambayo wataona hawajatendewa haki, Umuhimu wa vyama vya wafanyakazi, Taratibu za malipo ya mafao katika mifuko ya kijamii, Nafasi ys kutembelea kivutio cha Ngorongoro n.k.


Katibu Mkuu TUGHE, Hendry Mkunda

Katika hatua nyingine Katibu huyo Watafanyia kazi maoni yote yaliyotolewa ikiwa ombi la kutaka Seminahiyo ya waaji na wafanyakazi iwe endelevu, kufanya maandalizo mapema Ili washiriki wengi waweze kuhudhuria.

“Maoni mliyotupatia tutafanyia kazi ili kuboresha maandalizi ya semina zijazo. Waajiri walioshiriki tunawashukuru wamejionea Chama cha wafanyakazi sehemu ya kazi sio adui bali kinaleta ushirikiano baina ya pande mbili. Niwaombe kafundisheni wenzenu haya mliojifunza. Makatibu humu ni wengi, Tunataka kuona mabadiko na maboresho na tutafuatiliana kuona. Mabaraza yaende kuboreshwa kiutendaji” Katibu Mkuu TUGHE.


Sehemunya Wajumbe wa semina ya siku tano iliyoandaliwa na TUGHE iliyohitimishwa rasmi Disemba 04 Jijini Arusha.

BY Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button