Habari

Rais wa Afrika Kusini amteua Mo Dewji kama mshauri wake wa uwekezaji

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amemteua mfanyabiashara kijana nchini, Mohamed Dewji (Mo) kuwa kwenye jopo lake la watu watano kumshauri kuhusu masuala ya uchumi na uwekezaji.

Tanzania billionaire Mohammed Dewji told kidnapper to shoot him - BBC News

Dewji, ambaye hivi karibuni Jarida maarufu la Forbes limemtaja kuwa bilionea kijana wa 13 kati ya 18 barani Afrika, ameingia kwenye jopo hilo ambalo lengo ni kupanga mikakati ya namna bora ya kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya Afrika Kusini.

Taarifa kwa vyombo vya habari jana, imeeleza kuwa Mo Dewji, anayemiliki kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (MeTL), atakuwa kwenye chombo hicho kwa kipindi cha miaka mitano.

Imesema kuwa uamuzi wa Ramaphosa kumteua Mo Dewji kuwa mshauri wake umetokana na kuvutiwa na jitihada za mfanyabiashara huyo maarufu nchini, kubobea kwenye masuala ya uchumi, huku akiifanya MeTL kuwa miongoni mwa kampuni bora Afrika.

Pia, uteuzi huo umeelezwa kuwa unatokana na Ramaphosa kuthamini na kutambua mchango wa Mo katika uwekezaji ambao umekuwa kichocheo kwa uchumi wa mataifa mbalimbali Afrika.

“Ninayo furaha kubwa kukujulisha kwamba, nimekuteua kwenye Baraza la Ushauri la Rais kuhusu uwekezaji ambalo lina jukumu kubwa kuhakikisha Afrika Kusini inapiga hatua kiuchumi na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents