HabariSiasa

Rais wa Burundi adai Rwanda ina mpango wa kuvamia taifa lake

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ameonya kwamba mzozo wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo unaweza kusambaa na kuwa vita vya kikanda.

Wanajeshi wa Burundi wamekuwa wakisaidia jeshi la Kongo kupambana na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, ambao hivi karibuni waliuteka mji wa Goma na wamekuwa wakielekea kusini.

Bw. Ndayishimiye alionya kwamba iwapo Rwanda itaendeleza kile alichokiita ushindi wake, vita vinaweza kusambaa hadi Burundi, jambo ambalo alisema halikubaliki.

Huku mvutano ukiwa tayari umetanda kati ya Burundi na Rwanda, Umoja wa Mataifa unaonya kwamba mapigano ya moja kwa moja yanaweza kuzua marudio ya vita vya kikanda yaliokuwa mwishoni mwa miaka ya 1990.

Burundi ilikata uhusiano na Rwanda mwaka jana, ikiishutumu kwa kuwahifadhi waasi walioshambulia eneo lake miaka miwili iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents