Rais wa Dunia Dental Confederation Kutua Tanzania Kwa Tanzania Dental Expo 2026

Kuelekea maonesho ya kimataifa ya vifaa tiba na huduma za afya ya kinywa na meno yajulikanayo kama Tanzania Dental Expo 2026, maandalizi yanaendelea kushika kasi huku tukio hilo likitarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Mei 28 hadi 30 mwaka huu.
Maonesho hayo yanatarajiwa kuwakutanisha madaktari bingwa, wataalamu wa afya, wadau wa sekta ya tiba pamoja na kampuni mbalimbali za vifaa tiba kutoka ndani na nje ya Tanzania, kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kuonesha maendeleo ya teknolojia ya kisasa katika huduma za afya ya kinywa na meno.
Akizungumza kuelekea tukio hilo, Dk. Mbege Mwakatobe ambaye ni daktari bingwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili National Hospital na Mkurugenzi wa Tanzania Dental Expo, amesema maandalizi yanaendelea vizuri huku ugeni mkubwa wa kimataifa ukitarajiwa kushiriki katika maonesho hayo.
Amesema miongoni mwa wageni muhimu watakaohudhuria ni madaktari bingwa, wawekezaji na wadau wa sekta ya afya kutoka nchi mbalimbali duniani, jambo litakalosaidia kukuza ubora wa huduma za afya ya kinywa na meno nchini Tanzania.
Dk. Mwakatobe amebainisha kuwa tukio hilo litapambwa zaidi na ujio wa Rais wa FDI World Dental Federation, Assoc. Prof. Dr. Nikolai Sharkov, ambaye anatarajiwa kuwa mgeni maalum katika maonesho hayo ya kimataifa.
Aidha, waandaaji wameeleza kuwa Tanzania Dental Expo itakuwa fursa muhimu kwa wataalamu wa afya kujifunza matumizi ya vifaa tiba vya kisasa, kujenga ushirikiano wa kimataifa pamoja na kuhamasisha maboresho ya huduma za afya ya kinywa na meno kwa wananch




