AfyaHabari

Rais wa Madaktari aunga mkono mgomo wa wafanyakazi wa afya Uganda

Rais wa jumuiya ya Madaktari nchini Uganda amesema anaunga mkono mgomo unaofanywa na wafanyakazi wa afya ambao wanaishutumu serikali kwa kutotengeneza mazingira bora ya kufanyia kazi ili kuweza kushughulikia mlipuko wa Ebola nchini humo.

Dr.Sam Oledo rais wa chama cha wafanyakazi nchini humo amesema wakati madaktari wako tayari kufanya kazi zao lakini wanahitaji kuwa salama kwanza. “ wafanyakazi wa afya wamevunjika moyo na wana wasiwasi. Wote walioko katika eneo la kufanyia kazi kwenye Ebola lazima wawe na vifaa vya kulinda usalama wao.” Idadi ya vifo kutoka na mlipuko wa Ebola nchini Humo imefikia 23 maafisa wa afya wamesema.

Bwana Emmanuel Ainebyoona , afisa wa habari mwandamizi amesema ripoti inaonyesha hali ya sasa kwamba kati ya watu 36 wanaodhaniwa wameambukizwa na Ebola, ni 18 hadi sasa wamepata uhakika wana virusi na kesi 18 hazijathibitishwa.

Wakati huo huo jamhuri ya kidemokrasia ya congo ilitangaza kwamba hakuna tena Ebola Mashariki mwa jimbo la kivu kaskazini , Waziri wa afya Jean- Jacquues mbungani Mbanga alisema katika taarifa jumanne.

Mlipuko wa 15 katika taifa hilo la Afrika ya kati umezuka wakati kesi mpya ya virusi hivyo vinavyouwa vilithibitishwa Mashariki mwa mji wa Beni Augusti 22.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents