HabariSiasa

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amtumbua makamu wake

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amemvua mamlaka yote aliyomkabidhi makamu wake Saulos Chilima baada ya kiongozi huyo kutajwa kwenye kashfa ya ufisadi iliyoligubika taifa hilo.

Uchunguzi wa madai hayo ya rushwa kwenye manunuzi unaofanywa na taasisi ya kupambana na rushwa, ACB umehitimsha kwamba maafisa 53 wa umma waliowahi na ambao bado wapo madarakani walipokea fedha kutoka kwa mfanyabiashara, raia wa Uingereza na Malawi Zuneth Sattar kati ya Machi na Oktoba, mwaka 2021.

Sattar anachunguzwa nchini Malawi na Uingereza dhidi ya madai ya rushwa na utakatishaji fedha. Kulingana na katiba ya Malawi, Chakwera hana uwezo wa kumsimamisha ama kumuondoa Chilima kwa kuwa ni afisa wa kuchaguliwa. Makamu huyo wa rais hakupatikana kuzungumzia hatua hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents