Siasa

Rais wa Mali: Jaribio la kutaka kuniua ni sehemu ya kazi yangu

Rais wa Mali amepuuzilia mbali jaribio la kumuua lililofanyika ndani ya Msikiti wakati wa sala ya Eid al-Adha – akisema kuwa”Ni sehemu ya kuwa kiongozi”.

“Kila kitu kiko sawa. Hakuna tatizo,” Assimi Goïta aliwambia waandishi wa habari, saa kadhaa bada ya wanaume wawili kumshambulia katika msikiti mkuu wa wa Grande Mosque uliopo katika mji mkuu Bamako.

Mmoja wa washambuliaji hao alikuwaamejihami kwa kisu, kulingana na ripoti, na alijaribu kumdunga rais.

Hatahivyo, alishindwa kumjeruhi Kanali Goïta, ambaye aliongoza jeshi kuchukua malaka ya nchi mwezi Agosti mwkaa jana, na wakakamatwa maramoja.

“Ni sehemu ya kuwa kiomngozi,” alisema rais huyo wa mpito na kuongeza kuwa. “Kuna watu kila mara ambao hawajafurahi, kuna watu ambao wakati wowote wanaweza kujaribu kufanya mambo kuyumbisha, kujaribu kufanya vitendo tofauti.

“Ninataka kuwahakikishia watu na kusema kuwa niko vyema, hakuna shida, hakuna aliyejeruhiwa na hali ilishugulikiwa .”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents