Rais wa Marekani Joe Biden atazuru Israel siku ya Jumatano, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza kutoka Israel.
Tangazo kwamba Rais Biden atazuru Israel lilitolewa katika ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem baada ya mkutano wa saa saba kati ya mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Antony Blinken na Waziri Mkuu Netanyahu siku ya Jumatatu.
Biden “atapokea taarifa za kina juu ya malengo na mkakati wa vita vya Israeli” wakati akiitembelea nchi hiyo, Blinken aliwaambia waandishi wa habari.
Pia “atasikia kutoka kwa Israeli jinsi itakavyoendesha operesheni zake kwa njia ambayo itapunguza majeruhi ya raia” na kuruhusu msaada kuwafikia raia wa Palestina huko Gaza.
Ziara ya Biden inawadia kwa mwaliko wa Netanyahu.
Biden kusafiri hadi Jordan baada ya Israeli
Msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa John Kirby anaanza mkutano wake na waandishi wa habari kwa kusema kuwa Rais Biden “atawasili katika wakati mgumu” katika mzozo kati ya Israel na Hamas atakapotua Tel Aviv, Israel siku ya Jumatano.
Malengo makuu ya Biden, anaanza, ni “kuthibitisha tena mshikamano wetu” na Israeli na kuwezesha misaada kwa raia huko Gaza.
“Atajadili suala la usaidizi wa kibinadamu” kwa njia ambayo hainufaishi Hamas, Kirby anasema, baada ya safari ya Biden kutangazwa mwendo wa saa 03:00 kwa saa za mjini Jerusalem.
Wasiwasi wa usalama kwa safari ya Biden
Uamuzi wa rais wa Marekani kusafiri hadi Israel “haukuchukuliwa kirahisi” anasema Kirby.
Hakushirikisha maelezo mengi lakini alisema: “Ni safari fupi sana”. Biden atatembelea Tel Aviv kwanza kabla ya kwenda Amman.
Wanadiplomasia wa Marekani waliozuru na wabunge wamelazimika kujikinga dhidi ya maroketi ya Hamas yaliyotua Israel katika siku chache zilizopita.