HabariSiasa

Rais wa Marekani Joel Biden alivyodondoka jukwaani

Rais wa Marekani, Joe Biden amepiga mweleka jukwaani wakati wa sherehe za kuhitimu za Chuo cha Jeshi la Wanahewa la Marekani huko Colorado siku ya Alhamisi.

Biden, ambaye alitoa hotuba ya kuanza na kupeana mikono na wahitimu, alianguka karibu na jukwaa na kusaidiwa haraka na walio karibu naye kusimama wima na kuondoka bila kusaidiwa huku akiendelea kuwasalimia watu kwenye sherehe hiyo.

Kwa mujibu wa waandishi wa habari waliokuwa wakisafiri na Rais, Biden (80) alijikwaa kwenye mfuko mweusi wa mchanga.

“Rais yupo sawa, Kulikuwa na mfuko wa mchanga jukwaani alipokuwa akipeana mikono,” Ben LaBolt, mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu ya Marekani, alitweet huku video za tukio hilo zikisambazwa mtandaoni.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents