Rais wa Olimpiki awapongeza wahudumu

Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki – IOC Thomas Bach, amewasifia wahudumu wa matibabu na wafanyakazi wa kujitolea kwa kufanikisha kuandaliwa Michezo ya Tokyo wakati huu wa janga la corona.

Amesema Michezo hiyo itatuma ujumbe mzito wa “amani na mshikamano.” Michezo hiyo iliyoahirishwa mwaka jana kwa sababu ya janga la virusi vya Corona, inaanza Ijumaa wiki hii lakini itakuwa bila mashabiki viwanjani baada ya uamuzi wa Japan mapema mwezi huu kuwa na viwanja vitupu ili kupunguza kitisho cha maambukizi.

Akizungumza katika kikao cha IOC pamoja na Waziri Mkuu wa Japan Yoshihide Suga, Bach amesema wakati Japan ilianza safari miaka 10 iliyopita ya kuleta Michezo ya Olimpiki mjini Tokyo, hakuna yeyote aliyeweza kufikiri kuhusu changamoto ambazo hazijawahi kutokea wanazokabiliana nazo kwa sasa.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button