HabariSiasa

Rais wa Taiwan ajiuzulu uenyekiti wa Chama

Kiongozi wa Taiwan Tsai Ing-wen, amejiuzulu wadhifa wa uenyekiti wa chama chake cha Democratic Progressive baada ya kupoteza viti kadhaa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mapema jana.

Tsai amesema atawajibika kwa kushindwa huko kwasababu aliteua wagombea walioshiriki uchaguzi huo wa mameya, wanachama wa mabaraza la jiji na viongozi wengine wa ngazi ya chini ya utawala katika kaunti zote 13 za Taiwan na miji tisa.

Pia kulikuwa na kura ya maoni kuhusu kupunguza umri wa kupiga kura kutoka 20 hadi 18.

Katika uchaguzi huo chama cha kikuu cha upinzani za siasa Kizalendo cha Kuomintang, kimepata ushindi wa viti 13 kati ya 21 vya umeya wa jiji na wakuu wa kaunti, ikiwa ni pamoja na mji mkuu, Taipei.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents