Habari

Rais wa Ufaransa abadili simu kwa hofu ya udukuzi

Hungary, Israel na Algeria zinachunguza madai kwamba programu ya kijasusi iliyotengenezwa Israeli ilitumika kuwadukua waandishi wa habari, wanaharakati wa haki za binadamu na wakuu wa nchi 14, wakati Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akilazimika kubadilisha simu yake na namba juu ya wasiwasi zaidi wa udukuzi.

Macron ambaye jina lake ni miongoni mwa wahanga wa sakata hilo, amemauru kuimarishwa kwa itifaki zote za kiusalama kufuatia kikao cha dharura cha baraza la taifa la usalama.

Shirika la Amnesty International na shirika la habari lisilo la serikali la Ufaransa la Forbidden stories kwa kushirikiana na makampuni mengine ya habari ikiwemo Washington Post, the Guardian na Le Monde walianika orodha ya watu waliolengwa.

Programu ya Pegasus iliyotengenezwa na kampuni ya Israeli ya teknolojia ya ujasusi wa kimtandao ya NSO ndiyo inatuhumiwa kufanya udukuzi huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents