HabariSiasa

Rais wa Ukraine akanusha kutaka kumuua Putin

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekanusha kuwa nchi yake ilifanya shambulio linalodaiwa kuwa ni la ndege isiyokuwa na rubani dhidi ya Kremlin, ambalo Urusi inasema lilikuwa ni jaribio dhidi ya maisha ya Vradimir Putin.

“Hatumshambulii Putin wala Moscow. Tunapigania kwenye eneo letu. Tunalinda vijiji vyetu na miji yetu,” alisema, akizungumza katika ziara nchini Finland.

Ofisi ya rais wa Urusi ilisema kuwa vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vilizidungua ndege mbili zisizo na rubani usiku.

Ilitishia kulipiza kisasi wakati na mahala itakapona ni muhimu kufanya hivyo.

Picha za video ambazo hajijathibitishwa zinazozunguka kwenye mtandao zinaonyesha moshi upipaa juu Kremlin – eneo kubwa la makao makuu ya serikali lililopo katikati ya mji wa Moscow – mapema Jumatano.

Video ya pili inaonyesha mlipuko mdogo juu ya jengo la seneti, huku wanaume wawili wakionekana kupanda kwa shida juu kabisa ya jengo hilo la bunge.

Ofisi ya rais wa Urusi ilisema Ukraine ilikuwa imejaribu kushambulia makazi ya Bw Putin yaliyopo ndani Kremlin na kuelezea shambulio hilo kama “kitendo cha ugaidi kilichopangwa na jaribio la kumuua rais”.

Maafisa wanasema kuwa droni mbili zilizolenga ofisi hizo za serikali zimezuiwa kwa kutumia rada za umeme, na kuongeza kuwa Rais Putin hakuwa kremlin wakati wa shambulio linalodaiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents