Rais wa zamani wa Peru na mkewe wahukumiwa kifungo cha miaka 15 jela

Rais wa zamani wa Peru, Ollanta Humala, amepatikana na hatia ya utakatishaji fedha na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.
Mahakama katika mji mkuu, Lima, ilisema kuwa Humala ilikubali fedha haramu kutoka kwa kampuni ya ujenzi ya Brazil ya Odebrecht ili kusimamia kampeni zake za uchaguzi mwaka wa 2006 na 2011.
Mkewe, Nadine Heredia, ambaye alianzisha chama cha Nationalist Party na Humana, pia alipatikana na hatia ya utakatishaji fedha na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15.
Heredia alipewa hifadhi na Brazil na atakuwa na njia salama ya kusafiri kwenda huko na mwanawe, wizara ya mambo ya nje ya Peru ilisema.
Waendesha mashtaka walikuwa wameomba Humala ahukumiwe kifungo cha miaka 20 jela na Heredia miaka 26 na nusu.
Baada ya kesi iliyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu, mahakama ilitoa uamuzi wake uliokuwa ukisubiriwa kwa muda mrefu siku ya Jumanne.
Humala alikuwepo wakati uamuzi huo unatolewa huku mkewe akisikiliza kupitia video.
Rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 62 na mkewe walikuwa wamekana kufanya makosa yoyote.