Michezo

Ramovic awavunjia awatemea nyongo Wachezaji wa Yanga

YANGA imekamilisha kazi ya kwanza ugenini kwa kuichapa Al Hila, kazi ya pili iliyobaki ni kuichapa MC Alger Jumamosi ya wiki hii pale Benjamin Mkapa, kisha kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
.
Kocha wa Yanga, Sead Ramovic ameuona ugumu uliopo mbele yake kuikabili MC Alger, hivyo ametaja mambo ambayo yatafanikisha jambo hilo na kuwapa furaha Wananchi
.
“Hii mechi (dhidi ya Al Hilal) imekwisha, niliwaambia wachezaji baada ya kutoka ndani ya uwanja kila mmoja asitishe furaha yake, tunatakiwa kujiona kama hatujafanya kitu na tukitakiwa kwenda kufanya kitu kikubwa zaidi kwenye mchezo ujao wa nyumbani,”
.
“Tunatakiwa kushinda mechi ya mwisho kwa nguvu licha ya kwamba haitakuwa rahisi, MC Alger nao wanapitia mabadiliko kwenye timu yao tofauti na walivyoanza mechi za makundi, tunachotakiwa ni kuongeza umakini kwenye mechi hii ya mwisho.
.
“Tutakuwa nyumbani na wao walishinda dhidi yetu wakiwa kwao, tumekuwa na mabadiliko mazuri ndani ya timu yetu tofauti na mechi mbili za kwanza tulizocheza na tumeanza kuimarika kwa nguvu, nawapongeza sana wachezaji wangu, lakini wanatakiwa kutambua tunakwenda kucheza mechi ngumu itakayobeba heshima yetu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents