Rapa T.I akamatwa Amsterdam, ajirekodi ndani ya kituo cha polisi (+video)

Rapa kutokea Nchini Marekani Clifford Harris Jr T.I, alikamatwa siku ya jumanne, Agosti 3, huko jijini Amsterdam baada ya baiskeli aliyokuwa akiiendesha kugongana na gari la polisi na kuvunja kioo cha gari kinachofahamika kama ‘’side mirror’’.

Rapa huyo alijirekodi video akiwa ndani ya gereza katika mji mkuu wa Uholanzi huku akielezea sababu ya kukamatwa.

Rapa huyo alisema hivi,

“Ni wazi kwamba sikutakiwa kuwa na simu yangu wakati ninaendesha baiskeli na kuvunja kioo cha pembeni  ‘’side mirror’’ ya gari la polisi.

Aliongeza kwa kusema ”Bado sijakasirika nina wakati mzuri. Walinikamata na hawakunitia hata pingu. Walifungua tu mlango wa nyuma ya gari lao na Kisha nikialazimika kuingia.”

T.I. mwenye jina halisi Clifford Harris Jr, alisema kukaa kwake katika vituo vya polisi ni sehemu ya utamaduni wa nchi hiyo.

Hivi sasa  T.I. yuko Uholanzi kwa ajili ya kusherekea miaka 11 ya harusi na mkewe Tameka Cottle.

Na Raheem Rajuu.

Related Articles

Back to top button