Ray C kumtembelea Rais Kikwete Ikulu kwazua hisia tofauti

Ni ngumu kumfurahisha kila binadamu. After all, nobody is perfect. Jana mchana mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C alienda katika Ikulu ya Dar-es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini humo.

Ray C alienda Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka Ikulu, Rais alimpongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.

Tukio hilo hata hivyo limepokelewa kwa hisia tofauti na wananchi huku wengine wakikikosoa kitendo hicho. Bongo5 imekusanya maoni ya baadhi ya wananchi hao waliokuwa na haya ya kusema:

Abdoul Karem Abdoul

Wa TZ hata mfanyiwe nini hamuoni. Alichokifanya Rais kina tatizo gani? Nyie wengine mnaoumwa mnataka msaada wa rais je mlimpa habari kwamba mnaumwa akawatosa? Matatizo mengine elezeni wazazi wenu c kila kitu kinamuhusu raisi. Hongera Prezidaa

John Bosco

Mbona kwa Sajuki hakujigusa? au kisa alikuwa mwanaume halafu cha kushangaza ray c yeye akijitakia hayo matatizo ye mwenyewe ila mr prez dar kwa kupenda………. kaamua kumsaidia ila kuna wagonjwa wasanii kama Vengu nk. kama vipi amtoe na Lulu kule alipo.

Massoud Asman Kasoro

Hata wewe hujakatazwa kumsaidia utakae, wabongo wanapenda lawama vingapi wamefanyiwa na bado wanalalamika .mwacheni ndo alivoamua yeye na nyie amueni mbona kwenye maharusi mnaifanya lazima kwa wagonjwa mnalalamika then akifa mnatoa nyingi kwa jeneza?

Vivica Peter

Amefanya poa sn, lkn asiingalie masuper star wako watu wengi wanataka msaada wake kungefunguliwa rehab ht kim ppl will pay lkn iwe less amount maana familia nyingi ni za kimaskini ndio wanaharibika…na mianya ya kuingiza dawa ibanwe maana haiwezi kufa lkn ipungue.

Josephine Stanley Kajembe

Rais amefanya kitu cha busara,lkn awaangalie pia vijana wengine walioathirika na madawa kitaa,sio awaangalie wasanii au watu maarufu,hongera Ray C kwa kukubali kutibiwa na usirudie tena mama,u r so cute

Enock Kihinger

Mtu kabwia mwenyewe leo anatibiwa kwa fedha za watanzania.., aalaah.. kuna wazazi kibao wanakufa kwa kukosa msaada wakat wa kujifungua… wajinga wanatetea ujinga!! Huyo Ray C ni mkubwa kwan hakutambua madhara ya kubwia unga?

Aggrey William

Kweli Sanaa bongo hailipi, Ray c kaanza kuimba muda mrefu inakuaje akiugua mpaka asaidiwe matibabu, that means Hana Akiba

Fahim Seif

Tatizo la madawa ya kulevya ni janga la Taifa kama rais atafute chanzo cha kuingia madawa nchini na pawepo na sheria kali hata kunyongwa kwa wafanya biashara hiyo, na isitoshe kama ni Rais aangalie wangapi vjana wameathirika na madawa asichague mtu 1 hapo anamaanisha RC ni muhimu sana kwa watanzania kuliko rai wengine walioathirika na madawa ya kulevya, kama rais wa nchi bac saidia wote pia ondoa kwa nguvu zote madawa kama mnavyo waangamiza wanasiasa na waislam hapa Tz

SpaceAsnat Namtuli

Mi nadhani tusiwe na mitazamo -ve kila mara,wakati mwingine tuangalie suala liko hivi na tuache kama lilivyo,ukimpa m-tz suala alitazame atakachokueleza utatamani ardhi ipasuke uingie..binafsi nahisi RayC alikuwa maarufu na tatizo lililompata kila mtu alimwonea huruma though mateja wapo wengi but kila mtu ana bahati yake,only dat i can say

Related Articles

Back to top button