Rayon Sports yamtimua Kocha Robertinho

Uongozi wa Rayon Sports umeamua kuwasimamisha kazi Kocha Mkuu, Mbrazil Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’ na Kocha wa Magolikipa, Mazimpaka André, kutokana na matokeo mabovu ndani ya klabu hiyo.
Rayon Sports wameshinda mechi tatu pekee kati ya 10 zilizopita za Ligi na kushushwa mpaka nafasi ya pili baada ya kutoka sare ya 2-2 na Marine FC mnamo Aprili 5, 2025.
Taarifa zinasema kuwa, kitendo cha Mazimpaka kuendelea kumuamini kipa Khadime Ndiaye ambaye huwa anafanya makosa ni moja ya sababu zinazomfanya azidi kumuunga mkono Robertinho katika kipindi hiki ambacho wachezaji wanasema hawafanyi mazoezi ya kutosha na mabadiliko yake yanatia shaka.
Baada ya mechi 23 za michuano hiyo, Rayon Sports wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 47, pointi moja nyuma ya APR FC walio nafasi ya kwanza.