BurudaniHabari

Raysmuzik adondosha ngoma ‘YKTVBZ’ kupitia mixtape yake Night Owl

Staa wa muziki kutoka nchini Lagos Nigeria mwenye makazi yake jijini London mkali wa Afro-fusion, Raysmuzik
@raysmuzik ameachia ngoma yake ya ‘YKTVBZ’ ambayo amewashirikisha SK Golden Boy na Sarchebaby kutoka kwenye mixtape yake Night Owl.

Ngoma hiyo imefanywa na producer Jaylon ambaye amewahi pia kufanya kazi na Mr. Eazi na PsychoYP, lakini pia ‘YKTVBZ’ imepitia kwenye mikono ya producer Sparkzy, ambaye amechanganya na miondoko ya afrobeats na amapiano ndani yake.

Akizungumzia ‘YKTVBZ’, @raysmuzik amesema ”Wimbo huu ni wa kuburudisha zaidi na kuwafanya watu kuwa na furaha, pongezi kwa Sparkzy kwa kuufanya wimbo huu kuwa levo nyingine.”

‘YKTVBZ’ umepata sapoti kubwa kutoka BBC 1Xtra, Capital Xtra, The FADER and Complex na hivyo, RaysMuzik kuwa miongoni mwa wasanii wanaokuja kwa kasi nchini Uingereza.

For more information, interview or image request: [email protected]
To Find Out More About RaysMuzik, Go To: Spotify, Twitter, Instagram, Facebook,

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents