HabariSiasa

RC Arusha atoa tamko kuhusu kinachoendelea Loliondo

Mongella amewataka wananchi wa tarafa ya Loliondo Wilayani Ngorongoro kuwa watulivu kutokana na uchonganishi wa watu wasiokuwa na nia njema na nchi yetu

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Me.John Mongella,
amesema hayo leo June 11 2022 katika tarafa va loliondo wilaya ya Ngorongoro alipokuwa anaongea na vyombo vya habari kuhusiana na zoezi linaloendea la uwekaji mipaka katika wilaya hivo, Amewambia waandishi wa habari kuwa kuna baadhi ya watu na
mitaandao va kijamii kupotosha kuhusiana na kinachoendelea katika zoezi la uwekaji mipaka katika wilaya ya Ngorongoro.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.John Mongella amewataka wananchi Wa Tarafa ya Loliondo wilaya ya Ngorongoro Kuwa watulivu na kusikiliza maelekezo ya serikali katika zoezi la uwekaji mipaka.
Aidha amesema kuwa katika siku ya jana kulitokea kundi la watu wenye silaha ambapo askari wetu alijeruhiwa na kukimbizwa hosptal lakini alifariki dunia wakati anapatiwa matibabu.

Related Articles

Back to top button