HabariSiasa

RC Makalla aagiza wanaotupa takataka hovyo wazomewe

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema licha ya uwepo wa sheria na kanuni za kuwadhibiti wachafuzi wa Mazingira hususani wanaotupa taka hovyo ni vyema pia ikaenda sambamba na kuwazomea Kama sehemu ya kuwafanya wajisikie haibu kwa kosa walilofanya.
RC Makalla ametoa kauli hiyo leo wakati wa kikao kazi na Viongozi wa Wilaya wakiwemo Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Meya na maafisa mazingira kilichoketi kuweka mipango Bora ya Matumizi ya Ardhi kulingana master plan ya Mkoa na Mikakati endelevu ya Kuimarisha Suala la Usafi na utunzaji wa Mazingira.
Katika kikao kazi hicho kwa pamoja wamekubaliana kuweka Nguvu katika kusimamia Master plan ya mwaka 2020-2030 kwa kuhimiza utoaji wa vibali vya Ujenzi kwa wakati na utekelezaji wa Agizo la Wizara ya Ardhi kuhusu usitishaji vibali vya Ujenzi wa Vituo vya Mafuta.
Aidha RC Makalla ameelekeza watendaji kuanzia ngazi ya Mtaa kuhakikisha wanabeba jukumu la Usafi kwa kuweka Mkazo kwenye Kampeni ya Usafi wa Kila Jumamos ya mwisho wa mwezi na kudhibiti Machinga kufanya biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa.
Pamoja na hayo RC Makalla amewataka Wakandarasi wa utoaji taka kuhakikisha taka zinaondolewa kwa wakati na Wananchi walipe ada ya taka.
Hata hivyo RC Makalla ameelekeza Halmashauri za Mkoa huo kuangalia upya Suala la utoaji wa Mikataba ya muda mrefu kwa Wakandarasi wa Usafi ili waweze kukopesheka na kununua Vifaa vya kisasa tofauti na Sasa ambapo wanapatiwa Mikataba ya muda mfupi.
RC Makalla amesema tayari amefanikiwa kupata Dustbin za kutupa taka ambazo amepanga kuzigawa kwenye daladala na Vituo vya bus muda wowote kuanzia leo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents