Habari

RC Makalla: Atoa Wiki moja kukomeshwa biashara ya ngono Dar Es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa Wiki moja kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanadhibiti watu wote wanaofanya biashara ya Ngono kwenye eneo la Manzese Uwanja wa Fisi baada ya suala hilo kulalamikiwa na Wananchi.

Malalamiko hayo yametolewa wakati wa Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua Migogoro ya Wananchi Jimbo la Kinondoni ambapo wamedai kuwa imefikia hatua biashara hiyo inahusha pia utumikishaji wa kingono kwa watoto wadogo Jambo ambalo ni kinyume na sheria na maadili.

Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Jeshi la Polisi kuwatuma askari watakaovaa nguo za Kiraia na kuwanasa watu wote wanaofanya biashara ya ngono.

Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa kata na Mtaa huo kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kumaliza suala hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents