Afya

RC Makalla: Kuvaa barakoa kwenye chombo cha usafiri ni lazima na iwe level seat

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona ambapo amepiga marufuku Wananchi kuingia kwenye vyombo vya usafiri na sehemu za kutoa huduma pasipo kuvaa barakoa.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia Mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya ambapo amesema watafanya ziara za kustukiza kwenye Vituo vya Daladala, Feri, Stendi, Mabasi ya Mwendokasi, maeneo ya Masoko na sehemu zote za kutoa huduma ili kuangalia Utekelezaji wa agizo hilo.

Aidha RC Makalla amesema Serikali imejipanga kutoa huduma Bora za matibabu kwa wagonjwa wote watakaofika hospital na kuwataka Wananchi watakaoona dalili za Corona kuwahi vituo vya Afya.

Awataka LATRA kusimamia Level seat.

– Aelekeza Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya kusimamia Utekelezaji wa Mwongozo wa Wizara ya Afya

“TUNAKULINDA NA WEWE UTULINDE, VAA BARAKOA KWA MUSTAKABALI WA AFYA YAKO NA WENGINE.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents