RC Makonda akabidhiwa milioni 50 Zanzibar

Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) imetoa msaada wa hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni 50 kwa Mkuu Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.

Hundi ya fedha hizo zimetolewa na PBZ ikiwa ni ishara ya kuunga mkono jitihada za ujenzi wa ofisi 402 za Walimu katika Mkoa wa Dar Es Salaam.
Baada ya kupokea hindi hiyo, RC Makonda ameishukuru PBZ kwa kumuunga mkono katika kampeni yake ya ujenzi wa Ofisi za walimu.
Mkuu huyo wa Mkoa ameeleza kuwa fedha hizo alizopata kutoka Benki hiyo zitaenda kununua mifuko 50,000 ya Saruji itakayotumika kutengeneza matofali yapatayo 140,000 kwa ajili ya kujenga majengo hayo .
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo Juma Ameir Hafidhi amesema kuwa wameamua kutoa mchango huo kutokana na kazi anayoifanya RC Makonda kwa kuwa kazi zake zimekuwa sio za ubabaishaji hivyo wanauhakika fedha walizozitoa zitafanya kazi ikiyokusudiwa.
Vile vile Mkurugenzi huyo amemuhakikishia RC Makonda kuwa wataendelea kumuunga mkono kwenye shughuli za maendeleo.