Habari

RC Simiyu aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kulawiti aachiwa huru, vilio vyatawala mahakamani

Mahakama Kuu kanda ya Mwanza imemuachia huru aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk. Yahaya Nawanda katika kesi ya kulawiti iliyokuwa ikimkabili.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Erick Marley baada ya kupitia maelezo na vielelezo vya ushahidi.

Hakimu Marley amesema katika kesi hiyo ya jinai namba 1883/2024 , mahakama baada ya kupitia maelezo ya ushahidi na vielelezo imejiridhisha kuwa hakukuwa na muunganiko wa ushahidi unaoweza kumtia hatiani mshitakiwa na hivyo inamuachia huru.

Hata hivyo baada ya mshitakiwa huyo kuachiwa huru vilio vilitawala kwa ndugu wa Nawanda waliofika mahakamani hapo kuja kusikiliza hukumu hiyo.

Nawanda alikuwa akituhumiwa na shtaka la kumuingilia kinyume na maumbile (kumlawiti)  msichana ambaye ni mwanafunzi wa Chuo ambaye ni Tumsime Ngemela kosa ambalo alituhumiwa kulitenda June 02, mwaka huu eneo la maegesho ya magari Rock City Mall Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents