Real Madrid, Liverpool katika vita nzito dhidi ya Kylian Mbappe

Real Madrid inaamini kuwa mshambuliaji Kylian Mbappe ,21, atakuwa na mazungumzo nao kuhusu uhamisho kutoka Paris St-Germain. (Marca)

Liverpool ina mpango wa kumuuza beki wake Dejan Lovren,31, ingawa anatafuta kuongeza mkataba wake. (Goal)Kylian Mbappe

Bayern Munich wanajiandaa kuanza mchakato wa kumnasa Tanguy Ndombele ,23, wa Tottenham na Mfaransa mwenzie anayecheza katika nafasi ya kiungo cha kati katika klabu ya Monaco, Tiemoue Bakayoko,25. (Le 10 Sport via Daily Mail)

Manchester City itatoa ofa kwa kocha Pep Guardiola ya mkataba wa muda mrefu baada ya marufuku dhidi ya klabu hiyo kufutwa. (Mirror)

Pep Guardiola

Guardiola atapatiwa karibu kitita cha pauni milioni 150 kwa ajili ya kukipa nguvu kikosi cha City. (Guradian)

Nice imetoa ofa kwa kiungo wa kati Mhispania Rony Lopes anayekipiga Sevilla. (RMC Sport-in French)

Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Norwich Stuart Webber amesema kwamba kandarasi ombi la kutaka kumnunua mchezaji kinda mwenye kipaji mwisho wa msimu litaanza kwa dau la £20m . (Norwich Evening News)Mourinho na Tanguy Ndombele

Brentford inamlenga winga wa Portsmouth Ronan Curtis,24 kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Said Benrahma ikiwa ataondoka kwenye klabu hiyo. (The News, Portsmouth)

Related Articles

Back to top button