Real Madrid wapanga maangamizi mazito dhidi ya Arsenal leo hii

JE, REAL MADRID KUITOA ARSENAL KIUKATILI LEO??
Usiku wa leo ni Usiku unaosubiriwa kwa hamu sana na mashabiki na Wapenzi mbalimbali wa Soka, Je Usiku huu una nini??
Usiku wa leo ni mchezo baina ya Real Madrid dhidi ya Arsenal katika Dimba la Santiago Bernabeu ikumbukwe katika mchezo wa awali Real Madrid akiwa ugenini kwenye uwanja wa Emirates alipokea kipigo cha bao 3-0 dhidi ya Arsenal, kutokana na michezo mingine iliyochezwa usiku wa Jana ya Uefa Champions League timu nyingi zilizopoteza ugenini zimeambulia ushindi wakiwa nyumbani huku Barcelona nae aliyeshinda 3-0 akiwa nyumbani kwake akanusurika kutolewa baada ya Borussia Dortmund kuibuka na ushindi wa 3-1 akiwa nyumbani kwake.
Wadau wengi wa Soka walishuhudia pia mchezo kati ya Aston Villa dhidi ya PSG ambapo mchezo wa awali PSG aliibuka na ushindi wa 3-1 huku akiwa katika Dimba la Villa Park akakubali kichapo cha 3-2 hivyo tunaona kila mtu ashinde nyumbani kwake.
Mashabiki wengi wa Real Madrid wanaamini katika miujiza yao kutokana na Historia ya klabu hiyo, Real Madrid ishawahi kipindua meza dhidi ya miamba mikubwa zaidi ya Arsenal ikiwa pamoja na PSG, Manchester City, Bayern Munich, Borussia Dortmund n.k
Je unaiona Real Madrid ikifanya maajabu yake kama ilivyo kawaida yake, unaiona Arsenal ikifuzu kwenda Nusu Fainali usiku wa leo??
Mchezo huu unatarajiwa kupigwa majira ya saa 4:00 Usiku.
Imeandikwa na kuandaliwa @Johnbosco_mbanga