RECAP: Album ya Fid & Lord Eyez Je Imedoda?? (Video)
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameilizungumzia tukio la uzinduzi wa Album ya Fid Q na Lord Eyez ya NENO.
Anasema kuwa Ujio wa Album ya pamoja ya Fid Q na Lord Eyez itakuwa na impact kubwa sana kwenye upande wa kukuza na kuiridisha Hip Hop pale ilipokuwa.
Anasema moja ya kitu alichosikitika ni kwenye tukio la uzinduzi ambapo lilifanyika kwa udogo sana ukilingalisha na aina ya wasanii husika.
Anaongeza kuwa tukio hilo lingetakiwa kuwa kubwa sana kutokana na heshima ya Fid Q pamoja na Lord Eyez kwenye game ya Bongo Fleva, kitu ambacho kingesaidia hata kwenye uapnde wa Promo.
Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi??
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive
Cameraman & editor @samirkakaa