Burudani
RECAP: Alikiba ametoa somo la kuimba Live Zanzibar – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameichambua Show ya Alikiba ya kutimiza miaka 20 aliyoifanya Kendwa Zanzibar.
Anasema kuwa ukiachana na mapungufu mengine Alikiba ndio mkali wa Kuimba Show za Live Tanzania na Afrika Mashariki kwa sasa.
Ameimba zaidi ya masaa mawili Jukwaani lakini jamaa ametoa Show ya Standard ile ile na bado ameimba Live asilimia 80 ya nyimbo zake.
Mbali ya kuwa ni msanii kuna haja Alikiba awe anaelekeza au kuwafundisha wasanii wa sasa namna ya kuimba Live kwani wengi wao wana mapungufu makubwa mno.
@el_mando_tz ameichambua Show hii Youtube kwa urefu zaidi.
Cmaeraman & Editor @samirkakaa