RECAP: Alikiba apongezwe kwa Kuandaa Samia Cup – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amempongeza Alikiba kwa kuandaa
Samia Cup ambayo imechukua sura mpya kwa sasa.
Ukiondoa Ligi Kuu ya Mpira Tanzania inawezekana Samia Cup ndio yakawa mashindano yanayofuatiliwa zaidi kwa sasa
Tanzania ambayo yameandaliwa na Alikiba.
Mpaka sasa ni kumi la kwanza kwenye Mwezi wa Ramadhani lakini mashindano hayo yamekuwa kama ya mwezi mzima kwa namna watu wanavyoyapenda.
Hakuna tukio ambalo Mastaa wengi wamewahi kuonyesha upendo kama Samia Cup, kila aina ya Staa anatamini kufika pale kujionea.
Sio Mastaa tu hata watu wa kawaida wamevutiwa nayo na wanaenda kukutana na Mastaa wao pale Samia Cup.
Kwenye hili Alikiba apongezwe sana maana yalianza kama utani ila sasa yamekuwa kivutio kikubwa mno hapa Dar Es Salaam na nzhi nzima maana yapo Live Crown Media.
Karibia Mastaa wote wamefika ila wengi wanasubiria kumuona Diamond akienda kwenye tukio aliloandaa mpinzani wake Alikiba.
Unafikiri Diamond ataweza kwenda kushuhudia Samia Cup au bado upinzani wa Kibiashara wa moto licha ya kuwa baadhi ya wasanii wake wamefika pale kama D Voice na pia ndugu zake Diamond kama Ricardo Momo na Idd Santos.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongo5.