RECAP: Alikiba asilaumiwe Tommy Flavour na K2ga kuondoka Kings Music – El Mando
Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia wasanii wawili wa
Kings Music Tommy Flavour na K2ga kuondoka kwenye lebo hiyo.
Anasema kwenye hili Alikiba asilaumiwe kabisa tena apongezwe sana kwa kujitolea kuwasaidia wasanii bila kuwadai chochote kwa miaka yote ile.
Alikiba alitimia Platform zake ikiwemo page yake ya Instagram, jina lake na kila kitu chake kuwasaidia vijana ambao Tanzania ilikuwa haiwajui mpaka wakafahamika tena bila kuwadai chochote.
Kwa namna Alikiba alivyokuwa anawapambania wasanii wake kuna wengine walihisi Alikiba ana mikataba na wale wasanii lakini kumbe pale ni bure unaenda kujifunza muziki na kuondoka.
Sio kila msanii angeweza kutumia muda wake bure kuwapa nafasi vijana na kuwasaidia wafahamike lakini pia kuwapa collabo zote zile.
Tommy Flavour amenufaika sana na Alikiba kuliko hata K2ga, Tommy amepewa hit songs tatu na zote kubwa ila K2ga hana hata Collabo na Alikiba.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman @samirkakaa





