RECAP: Alikiba hajaitendea haki show ya miaka 20 – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz anasema kuwa Alikiba hajaitendea haki Show yake ya miaka 20 kw akukoseakana baadhi ya vitu.
Anasema kutimiza miaka 20 sio mchezo lazima angeandaa tukio la kuonyesha kweli msanii anatimiza miaka 20 kwenye game.
Kuna watu wengi sana ambao wamekuwa nyuma ya pazia kwenye muziki wa Alikiba kwa muda mrefu wangetakiwa kuwepo kwenye tukio.
Alikiba kama inawezekana airudie show hii Dar Es Salaam na afanye haya:.
– Kuandaa Documentary ya Alikiba ya miaka 20
– kumuika G Lover ambaye kamtoa mbali sana
– Kuwaalika KGT, Man Walter, Bob Junior
– Kumuika Seven Mosha
-Kumualika Mr Blue
-Kuwaalika Killy na Cheed
– Kurudisha kwa Jamii kwa kuandaa Event maalumu.
– Mashabiki wahojiwe waulizwe kuhusu ALIKIBA.
Kubwa zaidi Wawakilishi wa Wizara ya Sanaa pamoja na BASATA kutoa neno kuhusu miaka 20 ya Alikiba.
Anasema kwa upande wake anaona bado kuna vitu havijakamilika kuonyesha msanii kasherehekea miaka 20 ya Muziki wake.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yake ya YouTube ya Bongofive.
https://youtu.be/VfIP-LJus-I?si=wVpt-LrORiOYhBt8
Cameraman & Editor @samirkakaa