RECAP: Alikiba & Mbosso sio machawa wa Simba, Viongozi wa Yanga wapongezwe – El Mando
Kupitia kwenye kipindi chake cha @recap_mando @el_mando_tz amezungumzia Mbosso kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tukio la Simba day.
Anasema katika wasanii wanatakiwa kupongezwa ni Alikiba na Mbosso kwa namna wanavyofanya kazi na Simba, hawana uchawa bali wanafanya kazi tu.
Amempongeza Rais wa Yanga Injia Hersi kwa kumpatia Mbosso nafasi ya kutumbuiza kwenye Parade ya Yanga licha ya kuwa anajua kabisa Mbosso ni Shabiki wa Simba.
Katika kitu wasanii wengi wanatakiwa kunifunza ni namna Mbosso alivyoonyesha msimamo kwenye tukio la Yanga kwa kuangalia moyo wake unataka nini.
Hicho ndio kitu ambacho kinafanya Mbosso aheshimike na kupata nafasi ya kutumbuiza Simba day, hakuna msanii aliyewahi kupata nafasi kama ya Mbosso.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Camerman @mbanga






