Bongo MovieBongo5 ExclusivesBongo5 MakalaBurudaniDiamond Platnumz

RECAP: Baba levo kukaa meza moja na Alikiba na Diamond (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia ujio wa media mpya ya Baba levo Seven Media.

@el_mando_tz anasema Kuongezeka kwa media nyingi kuna faida kubwa sana kuliko hasara kwenye jamii kwani itaajiri vijana wengi sana.

Ameongeza kuwa Baba levo kwa sasa kwa upande wa Wasanii amekuwa msanii wa tatu baada ya Diamond na Alikiba wanaomiliki media zao.

Hii inaweza kuwa Baba levo baada ya kutoka Jela amepata somo kubwa sana la Maisha na hataki kurudi alipotoka kimaisha.

Baba levo ameeleza vision ya media yake lakini pia itakuwa ni media yenye utofauti mkubwa kwa namna alivyoeleza.

Kumuomba Diamond kuwekeza kwenye media yake ni njia ya kutafuta namna ya kujilinda zaidi pale atakapotetereka kimaisha kama itatokea.

Baba levo, Alikiba na Diamond wanakuwa ni wasanii wa kuigwa baada ya kuwekeza kwenye media.

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents