Bongo5 ExclusivesBurudaniMuziki

RECAP: Bongo Fleva imeanza kushuka?? (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia Show ya Comedy iliyoandaliwa na Jukwaa la Cheka Tu wikiendi ikiyopita.

Anasema kuwa kwa mara ya kwanza watu wameanza kushuhudia na kuiona nguvu ya Stand Up Comedy Tanzania kwa namna tukio lilivyojaza.

Ushawishi wa Comedy Tanzania umeongezeka mara dufu na hata kama ukiangalia kwa Wachekeshaji wenyewe utaona namna wanavyoendelea kupata heshima hapa nchini.

Mwanzoni ilionekana kama Wachekeshaji ni wqtu waliokosa la kufanya lakini Cheka Tu ilikuja kubadili mitazamo ya Watanzania na kuwafanya waamini kuwa hata Comedy ni Ajira.

@el_mando_tz anasema kuna namna Comedy imeanza kutishia uhai wa Bongo Fleva na huenda baada ya miaka miwili mpaka mitatu Comedy ikaja kuwa ndio Jukwaa kubwa zaidi Tanzania.

Show zao wanazofanya na viingilio vyao wasanii wachache sana wa Bongo Fleva wataweza kufikia level hiyo na hata wadau na viongozi wanavyoshawishika.

Unakubaliana na @el_mando_tz kwa asilimia ngapi na unahisi kwanini muziki umeanza kukosa ushawishi maana wasanii wachache ndio wana nguvu na wana uwezo wa kuandaa show zao??

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

 

 

 

 

 

 

Camerman & Editor @samirkakaa

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents