AfyaBongo5 ExclusivesBurudaniFahamuHabariLifestyleMakalaMarimba Music ChartMichezoSiasaTechnologyTragedy

RECAP: Comedi Tanzania imeshuka, wachekeshaji wameridhika hawana ubunifu – El mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia ukuaji wa Comedi Tanzania ambayo imeanza kupendwa kwa sasa.

Anasema kuwa kuna muda kila mtu alikuwa anapenda kwenda kwenye Events za Comedi Tanzania hasa Cheka Tu au Watubaki.

Ilifika muda watu walipata wasiwasi kuwa Comedi Tanzania inaweza kufikia ukubwa wa Bongo Fleva lakini Kwa sasa kuna namna imeanza kupoteza mvuto.

Kuna namna wachekeshaji wanaonekana kuridhika na mafanikio waliyonayo lakini pia kuonekana kukosa ubunifu maana hata content zimekuwa zile zile kila wakati.

Anasema kuwa moja ya kitu kilichopelekea hayo ni kukosekana kwa ushindani baina yao maana zamani ilikuwa kila mwaka lazima ingizo kubwa la wachekeshaji liongezeke kupitia Comedi Search.

Kwa sasa matukio hayo hakuna na ndio maana wachekeshaji wamebaki wale wale na wanajua wapo wao hata ubunifu kwa baadhi ya umepungua.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents