Bongo5 ExclusivesBongo5 MakalaBurudaniDiamond Platnumz
RECAP: Dah ya Nandy, Fallen ya Alikiba hii ndiyo Standard ya Kimataifa (Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia nyimbo ambazo zina sifa ya Kimataifa kutoka Tanzania.
Anasema mpaka sasa ni nusu ya mwaka yaani mwezi 7 nyimbo chache tu kutoka Tanzania ndio zina sifa ya kuwa International na zingine zimeshafanya vizuri tayari.
Ametaja baadhi ya nyimbo hizo kuwa ni Komasava ya Diamond, Hakuna Matata ya Marioo, Dah ya Nandy na Fallen ya Alikiba.
Mbali na hilo ameongeza kuwa kuna nyimbo ni kali sana lakini wasanii wengi hawafanyi Promo ya nyimbo zao.
Ukiacha hizo nyimbo alizotaja @el_mando_tz unahisi nyimbo zipi zina sifa ya kuwa za Kimataifa??
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.