BurudaniDiamond Platnumz

RECAP: Diamond ameitikisa Ghana kuliko Davido – El Mando

 

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia Tukio la Birthday la Richard Nii Quaye kutoka Ghana ambaye aliwaalika mastaa mbalimbali.

Anasema tukio hilo wasanii wawili tu ndio wamelofanya lika-Trend Afrika mzima na wasanii hao ni Diamond na Davido.

Lakini ukija kwenye wasanii waliokuwa kivutio zaidi Diamond alikuwa kivutio zaidi kuliko hata Davido na hata ukiona video nyingi yule Tajiri alikuwa karibu zaidi na Diamond.

Anasema Diamond kwa sasa ndio msanii pekee Afrika Mashariki aliyopo Active Kimataifa, siku aseme anaachana na muziki Tanzania tutabali weupe sana Kimataifa.

Hakuna hata msanii mmoja anayeinyesha Juhudi za Kwenda Kimataifa labda Rayvanny kidogo na bado anapambana.

Wasanii wengine wamelala sana inaonyesha wameridhika na hawataki mambo ya kufanya muziki wenye ushindani Kimataifa.

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Cameraman & Editor @samirkakaa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents