RECAP: Diamond amelisoma soko la muziki Duniani – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia ngoma mbili ambazo Diamond katoa na kashirikishwa.
Anasema Wasanii wengi wanachukulia poa Sound zetu lakini ukiusikiliza wimbo wa KUNA unagundua sisi tuna sound bora sana ya kimuziki.
Wasanii wanatakiwa kuzikibali na kuhakikisha wanatoa muziki wenye ubora kama KUNA, ule ni wimbo wenye Utamaduni wa Kitanzania na una sifa za Kimataifa.
Anapita kwenye njia za Akina Bi Kidude walifanya sound ya mduara na walifanya shows kwenye mataifa memgi Ulaya, ni sound yenye heshima yake.
Pia Diamond kuweka Verse kwenye ngoma ya My Darling wengi wanahisi Diamond kaweka verse kwa msanii mdogo lakini anajua kabisa soko linataka nini.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @samirkakaa