RECAP: Diamond amemfunika Ciara kwenye video yao – El Mando
Kupitia kwenye kipindi chake cha @recap_mando @el_mando_tz ameizungumzia video ya Ciara na Diamond ya Low.
Anasema wakati Audio inaachiwa ilionekana ya kawaida ila Video wameitendea haki na ndio imeubeba Wimbo mzima wa Low wa Ciara.
Anaongeza kuwa kwa namna hii lazima Diamond apewe sapoti sana maana anajipambania mwenyewe kufika pale alipo na wasanii wenzake wametulia.
Angalau msanii Rayvanny naye kuna sehemu anataka kufika ila asilimia kubwa ya wasanii wetu ni kawa wameridhika hakuna movement zozote wanazifanya Kimataifa.
Hii inaonyesha Kiwanda cha Bongo Fleva bado sana maana msanii mmoja au wawili ndio wanapambana kufika sehemu ila wengine hawaoni hata pakupita.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman @johnbosco_mbanga






