RECAP: Diamond amemkosea Zuchu?? amuombe msamaha??

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia kauli za Diamond kusema Zuchu sio mpenzi wake ni Msanii wake.
Anasema kuwa kama hiki kinachoendelea sio KIKI ya Ku-promote Reality Show basi Diamond amemkosea sana Zuchu.
Anaongeza inawezekana wasiwe wapenzi kweli ila kwenye Upande wa Thamani ya Zuchu atachukuliwa poa sana na wengine watdharau sana kutokana na kauli za Diamond.
Kitendo hicho linaweza kumpunguzia kasi ya Upambanaji na kujiona mpweke sana ukizingatia ile ni biashara yake.
@el_mando_tz anasema Reality Show maana yake ni kwamba kila unachofanya na kuongea ni ukweli, ni Uigizaji ambao asilimia 90 unachofanya ni ukweli wa maisha yako.
Kama Reality Show ni ukweli basi Diamond ameongea ukweli kwamba Zuchu sio mpenzi wake ni msanii wake, kauli zake zitafanya Zuchu ashuke thamani maana Kuwa na mahusiano na Diamond ilimpandisha sana Thamani.
Kwa maana hiyo Diamond amemkosea sana Zuchu, anastahili Heshima kubwa maana ni biashara yake ambayo inampa faida kubwa zaidi pale WCB.