BurudaniDiamond Platnumz

RECAP: Diamond amemtengeneza Jux anastahili tuzo – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia Jux kuchukua Tuzo ya msanii bora Afrika Mashariki Nigeria.

Anasema watu walianza kulalamika baada ya Jux kuchukua Tuzo mbele ya wasanii kama Diamond na Bien lakini kwenye Trace pia alichukua Tuzo ya msanii bora Tanzania mbele ya Diamond tena.

Anasema kuwa Ukweli ni kwamba tangu mwaka 2025 Uanze ukisema Diamond ni msanii bora kwa sasa utakuwa umekosea pakubwa sana.

Jambo lisilopingika ni kwamba Diamond ni msanii mkubwa sana Afrika ila kwa sasa Tanzania huwezi kusema msanii bora kutokana na wasanii wengine walivyotoa ngoma na zimekuwa kubwa.

Ngoma za Diamond kama Holiday na Kuna hazijafanya vizuri kama God Design na Ololufe Mi za Jux.

Anaongeza kuwa Ukubwa wa Jux wa sasa Diamond amechangia kwa asilimia 80 maana Collabo alizofanya naye ndio zimemkuza Jux.

Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.

Editor @samirkakaa

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents